×

Mahakama Kuu Yatupilia Mbali Ombi la Mbunge wa Kisesa Mpina

Mahakama Kuu, Masijala ya Dar es Salaam, imetupilia mbali ombi lililowasilishwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina la kuomba Mahakama hiyo imruhusu awasilishe majibu ya nyongeza katika kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na mwanasiasa huyo dhidi ya Waziri wa Kilimo, Waziri wa Fedha pamoja na taasisi tano, zikiwemo kampuni.

Mahakama imetoa uamuzi huo umetolewa Jumatano Septemba 18, 2024 na Jaji Arnold Kirekiano anayesikiliza shauri hilo, baada ya kukubaliana na mapingamzi yaliyowekwa na Serikali pamoja wajibu maombi wengine walioomba Mahakama hiyo isitoe nafasi hiyo kwa waleta maombi (Mpina) kuwasilisha mahakamani hapo majibu ya nyongeza.

Mpina amefungua shauri hilo la kikatiba namba 18383/2024, akipinga mambo kadhaa, ikiwemo uamuzi wa Waziri wa Kilimo kutoa vibali vya ununuzi wa sukari kupitia Bodi ya Sukari kwa kampuni ambazo hazimiliki viwanda vya sukari wala sukari.

Shauri la Msingi, mbunge huyo anapinga uamuzi wa Waziri wa Kilimo kutoa vibali vya ununuzi wa sukari kupitia Bodi ya Sukari kwa kampuni ambazo hazimiliki viwanda vya sukari wala sukari.

Pia, anapinga Waziri wa Fedha kuruhusu Kamisha wa Mamlaka ya Mapato (TRA) kuamuru kampuni za vocha kuingiza sukari nchini bila kulipa kodi na kupelekea Serikali kupoteza mapato ya zaidi ya Sh1.548 bilioni.

Vile vile, amezishtaki kampuni za sukari kwa kukubali kuingiza sukari na kukubali kupewa msamaha wa kodi.

Leave a Comment