
Mkurugenzi wa Mji amepata kibali kipya cha ajira kwa ikama ya mwaka 2023/2024 chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25.06.2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kufuatia kibali hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu anakaribisha
maombi kwa watanzania wenye sifa za kujaza nafasi za kazi zifuatazo :-
-DEREVA DARAJA LA II- NAFASI (1)
-MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III- NAFASI (20)
-MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II- NAFASI (3)
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 30 Septemba, 2024