×

Hatma Ya Dhamana Ya Mwanachama Wa Chadema Boniface Jacob Kujulikana Leo

 

 

HATMA ya dhamana ya Mwanachama wa Chadema, Mgombea nafasi ya Kanda wa Chama hicho na Meya wa zamani wa Ubungo jijini Dar es Salaam, Boniface Jacob, maarufu mitandaoni kama Boni Yai inatarajia kujulikana leo Jumatatu, Septemba 23, 2024, wakati Mahakama itakapotoa uamuzi wa maombi ya Serikali ya kuzuia dhamana yake.

Mwanasiasa huyo mkazi wa Mbezi Msakuzi, Dar es Salaam, anakabiliwa na kesi ya kuchapisha taarifa za uwongo kwenye mitandao ya kijamii.

Alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Dar es Salaam, Kisutu Alhamisi Septemba 19, 2024 na akasomewa mashitaka mawili, ambayo hata hivyo aliyakana.

Katika kesi hiyo Boni Yai anakabiliwa na mashitaka mawili yakiwamo kuchapisha taarifa za uwongo katika mfumo wa kompyuta katika akaunti ya X yenye jina la Boniface Jacob @Ex MayorUbungo kwa nia ya kupotosha umma kinyume na kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Kimtandano namba 14 ya mwaka 2015.

🔴#Live: MAANDAMANO ya CHADEMA – HALI ILIVYO DAR – POLISI WAMETANDA KILA KONA…

Leave a Comment