Rais Samia Acheza Mchezo wa Asili wa Bao na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas
Global Publishers September 23, 2024 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akicheza mchezo wa bao na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro wakati alipotembelea mabanda ya Maonesho katika uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma tarehe 23 Septemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amecheza mchezo wa asili wa bao na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas
Ndumbaro wakati wa kilele cha Tamasha la Utamaduni la kitaifa lililofanyika Songea mkoani Ruvuma leo
Septemba 23, 2024.
Rais Samia akiwa ameanza ziara yake Mkoani Ruvuma leo, alikuwa mgeni rasmi wakati wa kufunga Tamasha la Tatu la Utamaduni la Taifa.
Rais Samia akiwasili katika uwanja wa Majimaji mjini Songea kwa ajili ya kufunga Tamasha la Tatu la Utamaduni la Kitaifa mkoani Ruvuma tarehe 23 Septemba, 2024.Rais Samia akitembelea mabanda ya Maonesho kwenye Tamasha la Tatu la Utamaduni la Kitaifa lililofanyika katika uwanja wa Majimaji mkoani Songea tarehe 23 Septemba, 2024.
Rais Samia akiwa na Watoto wawili juu ya gari wakiwapungia mkono Wananchi wa Songea mara baada ya kufunga Tamasha la Tatu la Utamaduni la Kitaifa lililofanyika katika uwanja wa Majimaji mkoani Songea tarehe 23 Septemba, 2024.