×

Rais Samia ateua wenyeviti wa bodi mbalimbali

Rais Samia amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi mbalimbali ambapo amemteua David Chimbi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Balozi Dkt. Aziz Ponary Mlima kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO).

Rais amemteua pia Balozi Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Salim Milanzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Balozi Valentino Longino Mowola kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano (UCSAF), Kanali Mstaafu Joseph Leon Simbakalia kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu wa Mitambo (TEMDO) na Prof. Neema Mori kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa kipindi cha pili.

Leave a Comment