×

Mgombea urais wa Republican, Donald Trump kukutana na Zelensky

Mgombea huyo wa urais wa chama cha Republican, Donald Trump amesema atakutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky mjini New York siku ya Ijumaa katika jengo la Trump Tower.

Mkutano huo unatazamiwa kuendelea licha ya ripoti za awali kuwa ulifutwa huku kukiwa na hasira kutoka kwa wana Republican baada ya Zelensky kutembelea jimbo muhimu la Marekani la Pennsylvania.

Siku ya Alhamisi, Zelensky alikutana na Rais wa Marekani Joe Biden na Makamu wa Rais Kamala Harris katika Ikulu ya White House kujadili “mpango wake wa ushindi”, ambao anatumai utaishinikiza Urusi kukubali kumalizika kwa vita hivyo kidiplomasia.

ORUMA AMCHAMBUA NJE NDANI ATEBA na GOLI ALILOFUNGA – MBINU za KOCHA wa SIMBA – ”NAOGOPA”

Leave a Comment