×

Naomi Campbell Apigwa Marufuku kuwa Mdhamini wa shirika la kutoa Misaada

Naomi Campbell (54)

MWANAMITINDO Naomi Campbell (54) amepigwa marufuku kuwa mdhamini wa shirika moja la kutoa misaada baada ya uangalizi kugundua kuwa fedha za shirika hilo zilitumika katika hoteli za kifahari na kwa huduma za saluni.

Uchunguzi wa Tume ya shirika hilo uligundua kuwa shughuli za maonyesho ya mitindo kwa ajili ya usaidizi hazikufanyika kwa kiasi kikubwa cha pesa kilichopatikana kama ilivyotakiwa.

Badala yake zilitumika kwa ununuzi wa sigara na usalama wa Campbell na malipo mengine ambayo hayajaidhinishwa kwa mmoja wa wadhamini wenzake wa shirika hilo.

Amepigwa marufuku kujihusisha na shirika hilo kwa miaka mitano huku wadhamini wengine wawili, Bianka Hellmich na Veronica Chou, wakipigwa marufuku kwa miaka tisa.

MAKUBWA: MAMA KUNGWI LOVE – “PIPI KIFUA KICHOCHEO kwa MWANAMKE na MWANAUME – MUME WANGU NAMPA TENDA”

Leave a Comment