
MSANII mkongwe wa nyimbo za Injili kutoka Afrika Kusini, Solomon Molokoane, almaarufu Solly Moholo, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 65, wasimamizi wake wametangaza.
Mwanamuziki huyo aliyeshinda tuzo alikuwa amelazwa hospitalini kwa wiki kadhaa baada ya kuugua akiwa katika ziara ya muziki nchini Botswana mwezi uliopita.
Alipata umaarufu mwanzoni mwa miaka ya 2000 na kuwa jina maarufu katika muziki wa injili wa kitamaduni wa Afrika Kusini.
Wasimamizi wake walisema atakumbukwa sana kwa muziki wa uponyaji aliotupa kwa miaka mingi.
Mwezi uliopita, timu ya Moholo ilisema alipatwa na kiharusi na kwamba viungo kadhaa mhuhimi wilini mwake vimeacha kufanya kazi.