×

Mzee Warioba Afunguka Kuhusu Uongozi Wa Rais Samia, Wapinzani Kuandamana – Video

Aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jaji Joseph Warioba

WAZIRI Mkuu Mstaafu  na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jaji Joseph Warioba, amesema bado anayaona mafanikio ya falsafa ya Rais Samia Suluhu Hassan, ya R nne (4R) anazozitumia katika utawala wake na kuifanyia nchi kuwa katika utulivu.

Aidha amesema falsafa ya maridhiano (Reconciliation), Mabadiliko (Reforms), Ustahimilivu (Resilience) na Kujenga upya (Rebuilding), inaendelea kufanya kazi licha ya kuwapo changamoto chache hasa kisiasa.

Warioba amesema hayo leo Oktoba 4, 2024, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam, na kwamba kwa sasa nchi imetulia kisiasa tofauti na miaka mitatu iliyopita.

Amesema changamoto za kisiasa ni kama kuna mapambano kwa serikai na wapinzania ambao hawawasilishi hoja ipasavyo, huku akishauri wanasiasa kukaa meza moja kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Leave a Comment