×

Mbunge Deo Mwanyika Atunukiwa Tuzo Kata ya Njombe Mjini

 Uongozi wa Kata ya Njombe Mjini umeandika historia kwa kutoa Tuzo ya pongezi kwa Mhe. Mbunge kwa kutambua na  kuthamini mchango mkubwa wa maendeleo anaofanya  katika    kata ya Njombe Mjini na Jimbo zima la Njombe Mjini.
Akiongea baada ya kutunukiwa Tuzo hiyo. Mhe. Deo Mwanyika (MB) amewashukuru sana uongozi wa kata ya Njombe Mjini kwa tuzo hiyo. Tuzo hiyo inampa hamasa ya kuwa wananchi anaowatumikia wanatambua na kuthamini utumishi wake kwao.
Pamoja na mambo mengine, pia Mhe. Mbunge amebainisha shughuli mbalimbali za maendeleo ambazo serikali ya awamu ya sita ikiongozwa na Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan  imetekeleza katika Jimbo la Njombe Mjini katika sekta ya Afya, Elimu, Barabara, Umeme, Maji, Kilimo, Mifugo pamoja na utawala bora kwa kuimarisha 4R.
Mwisho, Mhe. Mwanyika ametumia hafla hiyo kuwahimiza wananchi kujiandaa kujiandikisha na kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa ifikapo Novemba 2024.

Leave a Comment