
Hamisa Mobeto; ni mwamamama staa nchini Tanzania anayetajwa kuwa mwenye mvuto kuliko wote kwa sasa ameshinda tuzo ya ‘Brand Ambassador Bora’.
“Nina furaha na shukrani zisizo na kipimo! 🏆 Kushinda tuzo ya ‘Brand Ambassador Bora’ wa mwaka katika The 100 Best Brands Africa ni uthibitisho kwamba unyenyekevu, kujituma, na hamu ya kukua ndio msingi wa mafanikio.
Kila hatua ninayochukua inaendeshwa na shauku ya kuwa bora zaidi, kuwa na nguvu zaidi, na kuvuka mipaka. Asanteni kwa wote wanaoamini katika safari yangu ya mafanikio” amesema Hamisa Mobeto