Dkt. Biteko Aongoza Wananchi Bukombe Kujiandikisha Daftari La Mpiga Kura

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha katika vituo vya kujiandikisha wapiga kura ili waweze kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
Dkt. Biteko amesema hayo leo Oktoba 11, 2024 mara baada ya kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura katika Kituo cha Kujiandikisha Mpiga Kura cha Shule ya Msingi Bulangwa kilichopo Wilaya ya Bukombe, Mkoa wa Geita.
“ Ninawashukuru sana kwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ni jambo la muda mfupi ni imaani yangu kuwa mtamaliza kwa wakati ili muweze kwenda kuendelea na shughuli zenu,” amesema Dkt. Biteko.
Amesisitiza “ Zoezi hili linaanza leo hadi Oktoba 20, 2024. Wananchi wa Bulangwa mjitokeze waandikishaji wamejiandaa vizuri na tunataka tuone orodha ya watu wote ili muda ukifika muweze kupiga kura,” amesema Dkt. Biteko.

ALIYEHUKUMIWA KUNYONGWA AKIWA na MIAKA 18 AELEZA ALIVYOPATA MUME GEREZANI – ”SIWEZI KUVIFANYA”…

