×

Gamondi: Kesho tuna mechi ngumu ya Derby, lakini tunajua namna tunauendea mchezo – Video


Kuelekea kwenye mchezo wa Kariakoo Derby hapo kesho baina ya Simba na Yanga, Kocha Mkuu wa Yanga Sc Miguel Gamondi amesema kuwa kuna baadhi ya wachezaji wake muhimu atakaowakosa kwenye mchezo huo licha ya kugoma kuwaweka wazi ni mchezaji yupi na yupi atakaekosekana.

Gamondi ameyazungumza hayo kwenye mkutano na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar Es Salaam uliofanyika katika ofisi za mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu Soka NBC Tanzania Bara.

“Ni kweli kuna baadhi ya Wachezaji wangu muhimu ni Majeruhi hiyo ni kweli, ila ni nani na nani wameumia nadhani utaona kesho uwanjani”

Tuna furaha kubwa kuelekea kwenye ligi huku tukiwa na mchezo muhimu wa Derby. Tupo vizuri, tuna matumaini makubwa ya kufanya vizuri hapo kesho. Hatujabadilika sana kwenye maandalizi tumejiandaa kama ambavyo tumekuwa tukifanya hapo awali”

“Tumetokea kwenye wiki ya FIFA na mara nyingi tunapata changamoto kidogo ya maandalizi kwani wachezaji wetu wengi wanakuwa kwenye majukumu ya timu za TAIFA. Kwa mfano kuna wachezaji wamefika jana na wengine wanaingia leo kwa mantiki hiyo lazima upate ugumu kwenye maandalizi lakini tutafanya kila liwezekanalo”

“Tunawaheshimu wapinzani wote tunaocheza nao ligi kuu. Ni kweli kesho tuna mechi ngumu kwani ni Derby, lakini tunajua namna tunauendea mchezo. Kila mara nasema mimi huwa sitazami sana historia. Yaliyopita yamepita, malengo yetu ni kutazama yanayokuja mbele yetu.” amesema Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga Sc.

Leave a Comment