
Katika muendelezo wa jitihada zake za kuwezesha biashara za ndogo na za kati (SME), Benki ya CRDB imewezesha wafanyabiashara wazawa zaidi ya 50 walio katika sekta ya ujenzi kushiriki katika maonyesho ya kimataifa ya Canton Fair yanayofanyika katika jiji la Guangzhou nchini China.
Msafara wa wafanyabiashara hao umeongozwa na Mkurugenzi wa Wateja wa Awali na Kati wa Benki ya CRDB, Bonaventura Paul ambae amesema Benki ya CRDB inatambua mchango mkubwa wa biashara ndogo na za kati(SME) katika uchumi wa nchi na ndio mana benki imekua ikiweka nguvu kubwa katika kuwezesha biashara hizo.

Mbali na hilo, Bonaventura amesema kuwa uwepo wa miradi mingi ya miundombinu huku wakandarasi wengi wa kigeni wakichukua kandarasi hizo ni moja ya sababu kuu iliyopelekea Benki ya CRDB kuamua kupeleka wakandarasi katika maonyesho hayo makubwa duniani ili kuweza kupata uzoefu kutoka kwa wakandarasi wakubwa duniani na kufungua mashirikiano ya kibiashara.
Benki ya CRDB imekua na utaratibu wa kupeleka wafanya biashara katika ziara mbalimbali za kibiashara nje ya nchi kila mwaka ambapo katika miaka ya karibuni imeshapeleka wafanyabiashara katika nchi za Uturuki, India na Italia.