Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, akiwa na Balozi wa Ufaransa, Malika Berak, wakati alipomtembelea ofisini kwake leo.
DC Makonda akizungumza na wanahabari baada ya mazungumzo na balozi wa ufaransa.
Balozi Malika Berak (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa wanahabari juu ya ziara yake kwa DC.
Wanahabari wakifuatilia tukio hilo kwa umakini.
BALOZI wa Ufaransa hapa nchini, Malika Berak amemtembelea na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ofisini kwake kujadili miradi kadhaa iliyopo wilayani humo.
Akizungumza na wanahabari leo, Dc Makonda amesema katika mazungumzo na Balozi huyo, pamoja na mambo mengine, walijadili juu ya miradi miwili, ya uvuvi na ujenzi wa machinjio ya kisasa, yanayotarajiwa kujengwa eneo la Mabwepande, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Amesema mazungumzo ni mwendelezo wa kutafuta ufadhili ili kuhakikisha miradi hiyo miwili inakamilika ambayo itakapokamilika, itakuwa imetumia zaidi ya shilingi bilioni 15. Kuhusu mradi wa machinjio, Makonda alisema ni matokeo ya ziara yake nchini Ufaransa hivi karibuni ambako alijionea ubora wa machinjio tofauti na ya hapa nyumbani.
Na Denis Mtima/Gpl