Absa Ilivyohitimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja Ikiahidi huduma bora zaidi
Global Publishers October 21, 2024 0 Comments
SHARE THIS:
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser ( kulia ) akikabidhi cheti cha shukrani kwa Makamu wa Rais wa Kampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited (Metl ), Vipul Kakad ( wa pili kushoto) katika hafla ya kuhitimisha wiki ya huduma kwa wateja, jijini Dar es Salaam, leo. Kutoka kushoto ni Msaidizi wa Makamu wa Rais wa Metl, Shamma Dhrani na Mkurugenzi wa Wateja wa Makampuni wa benki hiyo, Nellyana Mmanyi. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser ( kulia ) akikabidhi cheti cha shukrani kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Tanganyika Christian Refugee Service, Irene Mpangile (katikati) katika hafla ya kuhitimishs maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa benki hiyo, Melvin Seprapasen. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser akihitimisha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja wa benki hiyo jijini Dar es Salaam, leo.