×

Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian Atoa Tamko Wanajeshi Waliouawa

Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian.

Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian ametoa salamu za rambirambi kwa familia za watu wanne waliouawa kwenye mashambulizi yaliyofanywa na Israel kwenye kambi kadhaa za kijeshi nchini humo.

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa X, Rais Masoud Pezeshkian ametoa rambirambi hizo na kueleza kuwa Iran itaendelea kujilinda.

Iran imesisitiza kuwa mashambulizi ya makombora ya Israel yamesababisha uharibifu mdogo huku ikiapa kuwa haina mipaka katika kisasi chake baada ya ndege za kivita za IDF kushambulia vituo 20 vya kijeshi Jumamosi.

“Maadui wa Iran wanapaswa kujua kuwa watu hawa jasiri wanasimama bila woga wakitetea ardhi yao na watajibu ‘upumbavu’ wowote kwa hekima na akili,” aliandika.

Jeshi la Israel lilisema ndege zake zililenga vituo ambavyo Iran hutumia kutengeneza makombora yaliyolengwa Israel, pamoja na maeneo ya makombora ya juu kwa juu.

Hakuna ishara kuwa maeneo ya mafuta au ya nyuklia yalilengwa, na Iran ilisisitiza kuwa mashambulizi hayo yalisababisha “uharibifu mdogo tu.”

WAZIRI NDEJEMBI ATOA UJUMBE MZITO KWA WATUMISHI WASIOKUWA WELEDI

Leave a Comment