
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amefungua Mkutano wa wakurugenzi na maafisa wa Utawala na Rasilimali watu, Maendeleo ya Jamii na Maafisa Mawasiliano na Uhusiano wa Umma katika Sekta ya Maji, Novemba 14, 2024 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika Mkutano huo amewasihi Wataalamu wa Utawala na Rasilimali watu, Maendeleo ya Jamii, Maafisa Habari na Uhusiano kutambua kuwa wana jukumu kubwa na muhimu la kuhakikisha kwamba dhamira ya Mhe. Rais ya kumtua mama ndoo ya maji kichwani inatimia.

Mwisho Amewataka pamoja na kufanya kazi kubwa, kuendelea kujifunza mambo mapya na kuthamini familia na jamii inayowazunguka.
