
Msemaji wa Hezbollah, Mohammed Afif ameuawa katika shambulizi la Israel mjini Beirut amethibitishwa na mkuu wa wanajeshi wa Lebanon.
Shambulio liligonga makao makuu ya chama cha kisiasa cha Baath katika eneo lina watu wengi la Ras al-Naba Jumapili hii ni kulingana na vyanzo vya habari vinavyomilikiwa na serikali ya Lebanon.
Afif ambaye ni mmoja wa wachache waliobakia wa kundi hilo alionekana mara ya mwisho Jumatatu wiki iliyopita akitoa taarifa katika kongamano la mashinani kusini mwa Beirut ambako kundi hilo limekita kambi.
Shambulio hili limeuawa watu 4 na kujeruhi 14 linajiri kufuatia kampeni ya Israel dhidi ya Hezbollah ambayo imeongezeka tangu mwishoni mwa mwezi Septemba.