×

Rais Dkt. Mwinyi Awasili Zimbabwe Kushiriki Mkutano Wa Dharura Wa Wakuu Wa Nchi Na Serikali Wa SADC

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ally Mwinyi amewasili Jijini Harare, Zimbabwe Novemba 19, 2024 kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika jijini Harare Novemba 20, 2024.

Alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege, Rais Dkt. Mwinyi alipokelewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Zimbabwe, Mhe. Virginia Mabhiza; Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe. Hellen Bangawe pamoja na viongozi mbalimbali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwemo Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, IGP mstaafu Mhe. Simon Sirro.

Mkutano huo ambao umeshafanyika katika ngazi za maafisa waandamizi na mawaziri, utajadili masuala ya amani, ulinzi na usalama katika ukanda wa SADC na masuala mengine ya kuimarisha mtangamano wa kikanda.

Mhe. Rais Dkt. Mwinyi ataongoza pia Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Utatu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama unaotarajiwa kufanyika siku hiyo hiyo ya tarehe 20 Novemba, 2024.

MWANAFUNZI KIDATO CHA 2 AFARIKI DUNIA BAADA ya KUANGUKIWA na UKUTA wa SHULE AKISAIDIA UJENZI…

Leave a Comment