
Rais wa shirikisho la Soka Afrika (CAF), Dk. Patrice Motsepe atazuru Kenya, Tanzania na Uganda mwezi Desemba, 2024.
Kwa mujibu wa CAF, ziara hiyo inalenga kutathmini maendeleo na utayari wa viwanja na miundombinu mingine na vifaa kwa ajili ya kuandaa michuano ya CAF ya African Nations Championship (CHAN) 2025.
Kenya, Tanzania na Uganda watakuwa wenyeji wa michuano hiyo kuanzia Februari 1-28 mwaka 2025. Pia itakuwa ni mara ya kwanza kwa michuano ya CHAN kuandaliwa na nchi tatu.
Michuano ya CHAN ni ya wachezaji wanaoshiriki mashindano yao ya ligi ya ndani pekee.