×

Wananchi Wazidi Kunufaika na Magift ya Kugift, 7 Waondoka na Zawadi Mbalimbali Leo

Dar es Salaam 22 Novemba 2024: Kampuni ya mtandao wa simu ya Tigo, leo imewakabidhi wananchi zawadi ya simu janja aina ya Samsung washindi wawili na wengine 6 shilingi milioni moja kila mmoja baada ya kuibuka na ushindi kwenye kampeni ya ‘Magift ya Kugift’ inayoendeshwa na kampuni hiyo kwa ajili ya kuwarejeshea wateja wake sehemu ya faida waliyoipata.

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi zawadi hizo, Meneja Bidhaa wa Tigo, Eginga Mohamed amesema anayofuraha kukabidhi zawadi hizo ikiwa ni sehemu ya utaratibu wao kutoa zawadi mbalimbali kwa wateja wao.

Eginga amesema mpaka sasa wameshatoa zawadi za fedha zenye thamani ya  kiasi cha  TSh milion 24 kwa washindi wa makundi tofauti ikiwemo mawakala na wateja wengine.

Msemaji wa Kampeni ya Magift ya Kugift, Haji Manara (mwenye kanzu) akiwa katikati ya washindi waliokabidhiwa zawadi zao leo.

Kwa upande wake, Mwanaraph Muhidini ambaye amejishindia simu janja aina ya Samsung ameishukuru Tigo kwa zawadi hiyo kwani siku chache zilizopota alipotelewa na simu kama hiyo.

Hivyo amesema Tigo imerejesha tena furaha yake iliyotoweka tangu alipoibiwa simu hiyo.

Naye Ramadhan Idd mkazi wa Kinondoni ambaye ameshinda zawadi ya TSh milioni moja ameishukuru Tigo kwa kumuwezesha kupata pesa hizo ambapo amesema atazitumia kwa ajili ya kulipia ya ada ya shule kwa watoto wake.

Mercy Joseph ambaye ni Wakala wa Tigo Pesa ambaye amejishindia million moja ameelezea sababu ya kujishindia zawadi hiyo kuwa ni kufanya sana miamala hususani kwa upande wa huduma ya lipa kwa simu.

Hii ni wiki ya pili kati ya wiki 12 ambazo Tigo kupitia msimu huu wa sikukuu imepanga kutoa zawadi mbalimbali kwa wateja wake kupitia kampeni ya Magift ya Kugift.

Leave a Comment