×

Miti 1,000 Yapandwa Shule ya Sekondari ya Jangwani, ni Katika Uhifadhi wa Mazingira

Mkuu wa Mikakati na Uendelevu wa Benki ya NCBA akishiriki zoezi la upandaji miti kwenye Sekondari ya Jangwani Jijini Dar, Jumamosi iliyopita. Wengine ni wadau waliohudhuria kwenye tukio hilo.

Dar es Salaam, Tanzania – Novemba 30, 2024 – Benki ya NCBA Tanzania imefanikisha mpango wake wa kuendelea kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti 1,000 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani.

Shughuli hii, ikiwa sehemu ya dhamira kuu ya Benki ya kuendeleza mazingira endelevu, inachangia lengo la benki hii la mwaka 2024 la kupanda miti 6,000 kote nchini.

Tukio hilo la kupanda miti liliwaleta pamoja wanafunzi, walimu wa shule, na wawakilishi kutoka Benkiya NCBA, wakilenga kuboresha mazingira na kuyafanya yenye kijani kibichi na endelevu kwa shule hiyo na jamii inayozunguka.

Miti iliyopandwa itatoa kivuli, kuboresha bioanuwai, na kuimarisha ubora wa hali ya hewa, ikiwa ni ishara ya kujitolea kwa NCBA kukabiliana na changamoto za mazingira kupitia hatua madhubuti.

Akiwakilisha Benki ya NCBA, Mkuu wa Mikakati na Uendelevu, Bw. Charles Mbatia, alisisitiza kujitolea kwa Benki hiyo katika kujenga mustakabali endelevu. “Hapa NCBA, uendelevu ni msingi wa shughuli zetu. Kupitia miradi kama upandaji miti wa leo, tunaonyesha dhamira yetu ya kutunza mazingira ya Tanzania huku tukichangia jitihada za kuboresha maisha ya kila Mtanzania.

Kila mti unaopandwa unawakilisha ahadi yetu kwa serikali na kuifanya nchi yetu kuwa ya kijani zaidi ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Tukio hilo liliheshimishwa na uwepo wa mwakilishi wa serikali, lililoratibiwa na Mwenyekiti wa Rotary, Profesa Severin Rugumamu, ambaye aliisifu Benki ya NCBA kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha uendelevu. “Benki ya NCBA inatoa mfano mzuri wa jinsi biashara zinavyoweza kuchukua hatua za maana kuunga mkono uhifadhi wa mazingira huku zikijihusisha moja kwa moja na jamii wanazozihudumia,”alisema Mgeni Rasmi.

Shughuli hii inafuatia kampeni za awali za upandaji miti zilizofanywa na NCBA mapema mwaka huu. Benki iliunga mkono upandaji wa miti 1,000, Zanzibar kwa juhudi za uhifadhi wa Pwani, wakati huko Arusha, miti mingine 1,000 ilipandwa katika Hospitali ya Jiji la Arusha.

Mikakati hii inaonyesha dhamira ya NCBA katika uendelevu wa mazingira malengo ya kitaifa ya uendelevu wa nchi kiujumla.

Mbali na kupandamiti, Benki hiyo imeweka kipaumbele katika kuongeza uelewa kuhusu faida za uhifadhi wa mazingira. Katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani, wanafunzi walishiriki kikamilifu katika shughuli hiyo na waliweza kujifunza kuhusu jukumu muhimu la miti katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, kuhifadhi mifumo ya ikolojia, na kusaidia afya ya jamii.

Benki ya NCBA Tanzania itaendelea kujitolea kuunganisha uendelevu katika shughuli zake huku ikidumisha ushirikiano wao pamoja na jamii. Kwa kila mti unaopandwa, Benki inaimarisha nafasi yake kama kiongozi katika uwajibikaji wa shirika, ikileta athari endelevu za mazingira na kijamii.

Leave a Comment