×

Kampuni Yenye Internet Ya Kasi Zaidi Nchini Yatajwa na Kupewa Tuzo

Osama Nawayseh, Ookla Sales Director Middle East & Africa (kulia) akimkabidhi tuzo hiyo, CEO wa Kampuni ya Yas Tanzania, Jerome Albou.

Kampuni ya Mawasiliano ya Yas Tanzania imeshinda tuzo ya kuwa kampuni namba moja ya mawasiliano yenye mtandao wa Internet wenye kasi zaidi “Ookla Speedtest Award For The Fatest Mobile Network in Tanzania” ambapo kampuni ya Yas imeibuka mshindi wa kwanza kwa mwaka 2024 na kuziacha mbali kampuni zingine zinazotoa huduma ya mawasiliano nchini.

Akitangaza ushindi huo wa Yas Tanzania leo Jijini Dar es Salaam, CEO wa Kampuni ya Yas Tanzania, Bwana Jerome Albou amesema wamekuwa washindi wa tuzo hiyo kwa mwaka wa pili mfululizo na kwamba Yas Tanzania imepiga hatua kubwa sana kwenye kutoa huduma ya Internet yenye kasi zaidi nchini hivyo kukidhi vigezo vya kitaifa.

Aidha CEO, Jerome amesema Yas Tanzania imewekeza Jumla ya Trioni 1 za kitanzania katika kuhakikisha Tanzania Bara na Tanzania Visiwani kunakuwa na minara 4000 ya kiwango cha 4G huku wakiifikisha 5G kwenye miji yote mikubwa Tanzania.

“Yas Tanzania imedhamiria kubadilisha sekta ya mawasiliano kwa kuwapa wateja wake huduma za kisasa za kiteknolojia zinazohitajika sokoni kwa lengo la kukuza biashara, kuleta usawa na upatikanaji wa huduma jumuishi, ubunifu katika teknolojia na hivyo kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi” Amesema Jerome

CEO Jerome ameongeza kuwa wanapo sherehekea ushindi huu wa tuzo kutoka Okla bado wanazingatia jukumu lao la kutoa huduma bora katika sekta ya teknolojia ya mawasiliano nchini, na kwamba wamejiwekea malengo madhubuti ya kuongeza wigo wa upatikanaji wa mtandao imara na kuleta mapinduzi katika sekta ya digitali.

Akiwasilisha ripoti ya ushindi wa Yas Tanzania, Osama Nawayse kutoka Ookla amesema, kampuni ya Yas Tanzania imeshinda kwa asilimia 68.81 kwakuwa na Internet yenye kasi zaidi na hakuna kampuni yoyoye ya Mawasiliano Tanzania imefikia kiwango hicho.

Kwaupande wa medium dowloder speed Yas Tanzania imepata asilimia 43 ikizitangulia kampuni zote za mawasiliano nchini Tanzania sambamba na kuongoza katika vipengele vingine tofauti tofauti kuhusiana na masuala ya upatikanaji wa Internet yenye kasi zaidi nchini Tanzania.

Leave a Comment