The House of Favourite Newspapers
gunners X

Mkali wa Mitusi Kwenye Nyimbo nini Nay! Msome Eminem

0

naytrueboy

Nay wa Mitego

Na Chande Abdallah na Mtandao

WAKATI msanii Nay wa Mitego akijijengea jina kwa nyimbo zenye maudhui ya kuwachana au kuwatusi mastaa wenzake huku Wimbo wa Shika Adabu Yako ukipitiliza kiasi cha kufungiwa na BASATA, soma kidogo kuhusu mkali wa Rap kutoka Marekani, Marshall Mathers ‘Eminem’; Nay wa Mitego hamfikii hata robo kwa mitusi.Eminem-eminem-3

Eminem

Kwa mujibu wa mitandao ya kijamii nchini Marekani imeorodhesha watu zaidi ya mia moja waliotukanwa na Eminem kupita nyimbo zake huku kwenye idadi hiyo wakiwemo marais kama vile George Bush, Bill Clinton na makamu wake Chris Cheney.

Kama hiyo haitoshi Eminem ameshawahi kuwatukana watu muhimu katika maisha yake wakiwemo, mama yake mzazi, Debbie Mathers kwenye traki zake kama vile; Clean Out My Closet na My Mom huku akimuunganisha mke wake wa zamani, Kim kwenye Wimbo wa Kill You.

Baadhi ya mastaa aliowahi kuwatukana kwenye traki zake tofauti ni kama vile: Christina Aguilera, Britney Spears, Will Smith, Jessica Simpson, Rihanna, Kim Kardashian, Michael Jackson, Jarule, Dr Dre, Milley Cyrus, Mariah Carey, P Diddy na wengine kibao.

Leave A Reply