×

Freeman Mbowe: Nitagombea Nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA – Video

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema atagombea nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho ambao amekuwa akihudumu kwa takriban miaka 20.

Akiongea na Wahariri Jijini Dar es salaam leo Desemba 21, 2024, Mbowe amesema “Nimetafakari kwa kina sana, nimesema mara nyingi nilitamani kuondoka lakini siwezi kuondoka na minyukano ambayo ipo ndani ya Chama, kwahiyo CHADEMA nipo, nitakuwepo, nitagombea na mimi na viongozi wenzangu wanaoniunga mkono na wasioniunga mkono naamini tutakutana kwenye mazungumzo tuweke mambo sawa, sijawahi kuzuia Watu kugombea, anayetaka kugombea tukutane kwenye sanduku la kura”

Mbowe aliwaomba wanachama na baadhi ya viongozi wa CHADEMA kumpa saa 48 ili kuamua ikiwa atagombea nafasi hiyo, baada ya wanachama hao kukusanyika kwenye makazi yake kumshawishi agombee.

Leave a Comment