×

Rais wa Ufaransa Atangaza Baraza Jipya la Mawaziri

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron ametangaza Baraza jipya la Mawaziri ambapo amemteua Francois Bayrou kuwa Waziri Mkuu wake wa nne mwaka huu ili kuiondoa nchi hiyo kutoka kwenye mgogoro wa kisiasa.

Baraza hilo linajumuisha Mawaziri wa zamani ambao wamehudumu katika Wizara mbalimbali pamoja na watumishi waandamazi wa serikali huku wakitarajiwa kusimamia mchakato wa kupitisha bajeti ya mwaka 2025 ili kupunguza wasiwasi wa utulivu wa kisiasa barani Ulaya.

Majina ya baraza jipya la mawaziri yalisomwa na mkuu wa wafanyakazi wa ikulu Alexis Kohler ambapo amemteua aliyekuwa Waziri mkuu wa zamani Elisabeth Borne mwenye umri wa miaka 63 kuwa Waziri wa elimu, Waziri mkuu mwingine wa zamani Manuel Valls mwenye umri wa miaka 62, ameteuliwa kuwa Waziri wa maeneo ya nje yalio chini ya usimamizi wa Ufaransa huku aliyekuwa Waziri wa mambo ya ndani Gerald Darmanin akiteuliwa kuongoza wizara ya sheria.

Katika hatua nyingine, Eric Lombard mwenye umri wa miaka 66 ambaye ni mkuu wa taasisi ya uwekezaji wa sekta ya umma CDC ameteuliwa kuongoza wizara ya fedha huku Amelie de Montchalin akiteuliwa kuwa Waziri wa bajeti.

Baadhi ya mawaziri wameendelea kusalia katika nafasi zao wakiwepo Waziri wa ulinzi Sebastian Lecornu, Waziri wa mambo ya nje Jean-Noel Barrot, Waziri wa mambo ya ndani Bruno Retailleau pamoja na Waziri wa utamaduni Rachida Dati.

Baada ya baraza hilo kutangazwa Bayrou ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X kuwa & quot najivunia sana timu hii mpya tuliyoitangaza jioni hii.” Na kuongeza kuwa serikali yake yenye uzoefu imepania kurudisha tena imani.

LISSU AKISHINDWA ATAKUWA NANI NDANI ya CHADEMA?-MBOWE JE?/KIFO cha ALI KIBAO BADO GIZA NENE..

Leave a Comment