ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
Mlango ulifunguliwa polepole nikajua sasa kaka Cheni anawawasili si nikajiachia kwa raha zangu! Ili kudeka kwa kaka niliamua kugeukia ukutani ili akifika yeye ndiyo aniamshe kwa staili yoyote atakayoitaka, hata kunibusu au vyovyote vile.“Wewe umefungua mlango ili uende wapi au nani aingie muda huu?”
SHUKA NAYO MWENYEWE SASA…
Nilishtuka sana, nikakaa kitandani huku nikiweka sawa kanga kifuani ili kuziba nido zangu…
“Siendi mahali mama,” nilijibu huku nikiwa natetemeka pale kitandani.
Nilijiuliza mara mbilimbili, mama alikuwa amesimama wapi mpaka mimi nisijue kama hayupo ndani nyumba kubwa? Je, alikuwa anafuatilia mawasiliano yangu na kaka Cheni? Nilipata jibu kwamba hakuwa akifuatilia mawasiliano kwa sababu mimi simu yangu hainaga mlio hata siku moja.
Kaka Cheni yeye mlio wake uko chini sana. Hivyo isingekuwa rahisi kujua kwamba simu zetu ziko bize…
“Kwa nini sasa umefungua mlango halafu ukarudi kulala? Nani atakuja?” mama alinipiga swali la msingi sana…
“Hakuna mtu mama.”
“Sasa kwa nini umefungua mlango wako au unataka kuingiza wezi ndani?”
“Hapana mama, siwezi.”
Nilikuwa najibizana na mama huku moyoni nikisema angejua kwamba, kama angesubiri hata dakika mbili tu baada ya mimi kufungua mlango angemwona kaka Cheni anaingia chumbani kwangu, sijui ingekuaje!
“Njoo ufunge mlango haraka sana,” alisema mama huku akitoka. Akamwita kaka Cheni…
“We Cheni…”
“Naam…”
“Upo?”
“Nipo mama.”
“Haya.”
Mimi baada ya kufunga mlango nilirudi kitandani na kukutana na meseji ya kaka Cheni kwenye simu yangu…
“Mungu mkubwa,” aliandika hivyo…
“Mh! We acha tu,” nilimjibu.
“Nikupigie?” aliniuliza kaka Cheni kwa meseji…
“Piga,” nilimjibu baada ya kusikia mama akifunga mlango wa nyumba kubwa nikajua kaingia ndani…
Simu ikaita, palepale nikapokea…
“Yaani we kaka acha tu! Mh! Yaani sijui hata niseme nini? Hivi alikuwa wapi kwani?” nilisema mfululizo…
“Yule itakuwa alitoka na baba, wakati wa kurudi, baba akaingia yeye akabaki. Ila mimi namshukuru sana mungu maana kama angesubiri kidogo tu wewe ulipofungua mlango, angeniona nikiingia…”
“Na mimi niliwaza hivyohivyo kaka Cheni. Yaani leo sijui ingekuaje?”
“Mh! Unajua ulipofungua mlango tu, nikatoka kitandani mpaka mlangoni. Ndiyo nikamsikia na yeye akiongea.”
“Da! Sasa?” nilimuuliza kaka Cheni…
“Tulale, tutafanyaje sasa unadhani?”
“Aah! Lakini wazazi hawatutendei haki. Yaani wanatubana kiasi hiki kweli? Si sawa.”
“Si sawasawa kabisa. Hata mimi mwenyewe nashangaa sana. Ila tutaongea kesho, tulale,” alisema kaka Cheni akakata simu.
Nilijua kaka Cheni amekasirika sana. Maana hata ongea yake iliashiria hivyo. Sauti ilitoka kwa kutetemeka sana na huwa hivyo akiwa na hasira.
Nilikuwa nausaka usingizi kwa mbali, meseji kwenye simu yangu ikaingia baada ya kusikia simu ikitetemeka…
“Mimi sista iko siku nitahama hapa nyumbani na mtanitafuta sana hamtajua nimekwenda wapi!”
“Mh!” Nilimjibu kaka Cheni kwa kuguna tu.
“Mbona unaguna?” aliniuliza.
“Naguna kwa sababu ukisema uhame utapata faida gani sasa? We vumilia tu.”
“Haivumiliki sista. Kwa mfano hapa nilipo napenda ningekuwa na demu wangu kitandani na kibaridi hiki awe ananishika ananipa joto, lakini sasa sivyo.”
“Njoo nikupe joto,” nilimwambia kisha nikamsikilizia…
“We umeshayapuuza yaliyotokea?” aliniuliza.
“Mama hawezi kutoka tena. Ukitoka kwako funga mlango kwa funguo ili akija ajue umetoka kwenda nje ya nyumbani kabisa.”
“Oke, basi fungua mlango lakini kwa tahadhari kubwa sana, usilize kitasa,” kaka alinielekeza, nikamwambia sawa.
Nilitoka kitandani huku nikihakikisha hata kitanda hakitoi mlio wowote ule.
Nilifungua mlango, ile nafungua tu, kaka Cheni huyu hapa akaingia…
“Fungafunga haraka sana,” alisema.
Nilifunga mlango haraka sana. Tukaenda kitandani kukiwa na giza. Mimi nilimshika mkono…
“Wewe wa kwako umefunga?” nilimuuliza.
“Ndiyo…kwa funguo tena.”
Tulipanda kitandani. Kaka Cheni si alikuwa anataka joto, nikampa joto mpaka akawa anataka kuungua. Joto letu liliambatana na kucheza mechi. Tulipomaliza tukalala bwana. kumbe tulilala fofofo. Kuja kushtuka, kumekucha kabisa, mama anafagia nje…
“Chwaa…chwaaa…chwaa…” mlio wa fagio ulisikika.
“Kaka Cheni…kaka Cheni,”nilimwita kwa sauti ya chini akashtuka…
“Kumekucha na mama anafagia nje,” nilimwambia. Alifikicha macho ili ahakikishe mwenyewe, akabaini ukweli. Alikurupuka, akavaa harakaharaka na kuzama chini ya kitanda hata bila kuambiwa na mtu.
Ili kuweka usalama zaidi, mimi nilitoka kitandani, nikafungua mlango na kutoka nje…
“Shikamoo mama.”
“Marhaba. Umelala sana leo.”
“Ni kweli mama. Nilipitiwa.”
“Kaka yako hajaamka?”
“Sijajua mama.”
Mama aliacha fagio akaenda kwenye mlango wa kaka Cheni, akashika kitasa, ikaonekana mlango umefungwa…
“We Cheni,” mama aliita kwa sauti ya juu.
Je, kiliendelea nini? Usikose kusoma wiki ijayo.
Majanga..