×

Waziri Anusurika Kuuawa Baada Ya Kushambuliwa Kwa Risasi

Waziri wa Nchi anayeshughulikia bunge nchini Libya, Adel Juma amenusurika kuuawa baada ya watu wenye silaha kumshambulia akiwa ndani ya gari lake, tukio lililotokea jana Jumatano, Februari 12, 2025 jijini Tripoli.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) imelaani vikali shambulio hilo na kueleza kuwa itahakikisha wote waliohusika wanapatikana na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Waziri wa Nchi anayeshughulikia bunge nchini Libya, Adel Juma

Inaelezwa kuwa Adel Juma ni miongoni mwa washauri wa karibu wa Waziri Mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, Abdulhamid al Ddeibah aliyewekwa madarakani na Umoja wa Mataifa mwaka 2021 baada ya machafuko ya muda mrefu tangu utawala wa Muammar Gaddafi ulipoangushwa.

Matukio ya kuwashambulia maafisa wa serikali hiyo au ndugu zao, yamekuwa yakitokea mara kwa mara nchini Libya.