×

Nandy na Jux Wakabidhiwa Tuzo za Trace Johari Rotana, Dar

Faustina Charles Mfinanga, maarufu kama Nandy

Malkia wa Bongo Fleva, Faustina Charles Mfinanga, maarufu kama Nandy, na msanii nguli wa RnB kutoka Tanzania, Juma Jux, wamekabidhiwa tuzo zao za Trace usiku wa kuamkia leo, Machi 2, 2025. Hafla hiyo fupi imefanyika katika hoteli ya Johari Rotana, Dar es Salaam.

Msanii nguli wa RnB kutoka Tanzania, Juma Jux

Tuzo hizo zilicheleweshwa kutokana na changamoto za kimazingira, ambazo zilisababisha baadhi ya washindi kushindwa kuzipokea wakati wa hafla ya awali iliyofanyika visiwani Zanzibar hivi karibuni.

Nandy ametunukiwa tuzo ya Msanii Bora wa Kike, huku Jux akishinda tuzo ya Msanii Bora wa Kiume nchini Tanzania.