
Meridianbet Foundation, sehemu ya Golden Matrix Group (NASDAQ: GMGI), imezindua kampeni ya kimataifa ya uchangiaji vitabu, ambayo inalenga kusaidia maktaba ndogo na vituo vya jamii kwa kuwawezesha kupata vitabu vya elimu. Kampeni hii ni sehemu ya juhudi za Meridianbet Foundation kuhamasisha usomaji, kuimarisha elimu, na kuhifadhi utamaduni katika jamii mbalimbali duniani.
Wafanyakazi wa Meridianbet wamechukua jukumu la kujitolea na kuchangia vitabu walivyovisoma ili kuongeza rasilimali katika maktaba ndogo na vituo vya utamaduni. Kupitia kampeni hii, Meridianbet Foundation inataka kuhakikisha kuwa kila mtu anapata fursa ya kujifunza na kupata maarifa muhimu kwa maendeleo yao na ya jamii zao.
“Meridianbet Foundation inajivunia kusaidia maktaba ndogo, ambazo ni nguzo muhimu katika kukuza elimu na utamaduni. Kampeni hii ni hatua muhimu katika kuhakikisha kuwa watu wengi zaidi wanapata nafasi ya kusoma na kujifunza, bila kujali changamoto za kifedha zinazowakabili,” alisema Stefan Todorović, Mkuu wa Global CSR wa Meridianbet Foundation.
NB: Jisajili na Meridianbet na cheza michezo ya kasino ya mtandaoni upate ushindi kirahisi, Pia ongeza maokoto yako kwa kubashiri michezo mbalimbali yenye ODDS KUBWA. PIGA *149*10# AU tembelea tovuti yao meridianbet.co.tz
Kampeni hii itaendelea kuenea katika masoko yote ambako Meridianbet inafanya kazi, ikiwa ni sehemu ya dhamira ya kampuni kusaidia jamii kupitia elimu, utamaduni, na maendeleo ya kijamii.