×

Rais Samia Alivyowasili Arusha Kuongoza Maadhimisho Siku Ya Wanawake Duniani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluh Hassan amewasili Mkoani Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu na Viongozi wengine wa Chama na Serikali, kwenye kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro, asubuhi ya leo Jumamosi Machi 08, 2025.

Rais yupo Mkoani Arusha kuongoza Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayofanyika Kitaifa mkoani humo, kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Kauli Mbiu: Wanawake na Wasichana 2025; Tuimarisha Haki, Usawa na Uwezeshaji