×

Kaka wa Naomi Marijani Aanguka Akisoma Wosia wa Dada Yake – (Picha + Video)

 

Machozi na huzuni vimetawala nyumbani kwa Ismail Marijani, kaka wa marehemu Naomi Marijani, wakati wa kuaga jeneza lenye sampuli za viungo vya mwili wa dada yake, ambaye aliuawa kikatili na mumewe, Hamis Luwongo, huko Gezaulole, Kigamboni.

Naomi alifariki baada ya kushambuliwa na mumewe, ambaye alimuua kwa visingizio vya wivu na hasira. Baada ya mauaji hayo, mwili wa Naomi ulichomwa kwa kutumia magunia mawili ya mkaa, na kisha kupatikana majivu ya mwili wake.

Wakati Ismail alipokuwa akisoma wosia wa marehemu, huzuni kubwa ilimjaa na alijikuta akibubujikwa na machozi na kuanguka chini. Hali hiyo imewafanya wote waliokuwepo kumzunguka kwa kumfariji, huku majonzi yakiendelea kutawala.

Jeneza la Naomi limeagwa leo Mbagala Kijichi, jijini Dar es Salaam, ambapo familia, jamaa na marafiki walikusanyika kutoa heshima za mwisho kwa marehemu. Baada ya kuagwa, mwili wa Naomi umesafirishwa kuelekea Mwanga, Kilimanjaro, ambapo maziko yatafanyika kesho Jumamosi. Hukumu ya mume wa Naomi, Hamis Luwongo, alihukumiwa kunyongwa hadi kifo wiki iliyopita kwa mauaji hayo, ingawa familia inajua kuwa hata adhabu hiyo haiwezi kufuta maumivu ya kumpoteza mpendwa wao.