
Klabu ya RS Berkane wametawazwa mabingwa wa ligi kuu nchini Morocco kufuatia sare ya 1-1 dhidi ya US Touarga.
Kwa upande wa RS Berkane linakuwa kombe la kwanza la ligi kuu tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo.Klabu hiyo imewahi kutwaa kombe la shirikisho barani Afrika kwa mara ya kwanza mwaka wa 2020.
Ikatwaa makombe matatu katika msimu mmoja:Throne Cup,kombe la shirikisho Afrika na CAF Super Cup.
Imeweka historia ya kubeba kombe ikiwa haijafungwa katika michezo takribani 21 na kufungwa mabao kumi tu kwenye ligi kuu.