
Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Chanika SP Awadh Chiko umezikwa leo Machi 18, 2025 katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam kwa taratibu za kijeshi.
SP Awadhi Chico amefariki Dunia Machi 17, 2025 asubuhi kufuatia ajali ya gari iliyotokea eneo la Pugu Sekondari baada ya basi aina ya Eicher kugongana na gari la SP Awadh aina ya Prado wakati alipokuwa akielekea katika majukumu yake ya kila siku.

