
Raia wanne wa Canada wamenyongwa nchini China kwa mashtaka yanayohusiana na dawa za kulevya mapema mwaka huu, mamlaka ya Canada imethibitisha.
Wote walikuwa na uraia wa nchi mbili, na utambulisho wao umefichwa kwa ombi la familia zao, waziri wa mambo ya nje wa Canada Mélanie Joly aliwaambia waandishi wa habari jana Jumatano.
Alilaani mauaji hayo kama yasiyoweza kutenduliwa na hayaendani na utu wa msingi wa binadamu, akiongeza kuwa aliwaombea binafsi msamaha kwa serikali ya China.

Msemaji wa ubalozi wa China nchini Canada alisema ushahidi wa uhalifu wa raia hao wa Canada ulikuwa dhabiti na wa kutosha na kuitaka Canada ikome kutoa matamshi ya kutowajibika, kulingana na ripoti hiyo.
Ubalozi wa China pia umeongeza kuwa Beijing imehakikisha kikamilifu haki na maslahi ya raia wa Canada wanaohusika na kuitaka serikali ya Canada kuheshimu uhuru wa mahakama ya China.
Uchina haitambui uraia wa nchi mbili na inachukua msimamo mkali juu ya uhalifu wa dawa za kulevya.
Dawa kulevya zimekuwa zikipingwa katika nchi mbalimbali duniani na kuwekewa sheria kali ikiwemo sheria za kunyongwa au vifungo vya muda mrefu gerezani.