
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Machi 21, 2025, ameshiriki katika sherehe za uapisho wa Rais Mteule wa Namibia, Bi Nerumbo Nandi-Ndaitwah, zilizofanyika mjini Windhoek, Namibia.
Rais Nandi-Ndaitwah ni Rais wa kwanza mwanamke kuchaguliwa kushika wadhifa huo katika taifa la Namibia tangu nchi hiyo ilipopata uhuru wake tarehe 21 Machi, 1990.

“Tanzania na Namibia zimefanya kazi kwa bega kwa bega katika nyanja zote za maendeleo. Katika Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, nchi zetu mbili zimekuwa na mchango mkubwa katika kuendeleza masuala ya wanawake, uwezeshaji wa kiuchumi na usawa wa kijinsia,” alisema Rais Samia.
“Aidha, kwa Watanzania, tunafurahi kuona binti tuliyemlea na kumtunza kwa upendo na huruma sasa amepanda cheo cha juu kabisa katika ardhi hii ya Namibia. Mheshimiwa Rais, majirani zako wa Magomeni, Dar es Salaam, wanasherehekea na kukutumia salamu za heri.”
Kwa ndugu zetu wapenzi wa Namibia, Rais Samia alisisitiza, “Leo ni siku yenusiku ya uapisho wa Rais na pia ni siku ya Uhuru wenu. Asanteni kwa kuonyesha mfano mzuri wa kutumia haki yenu ya kidemokrasia kwa amani. Mmefanya chaguo la busara na uwekezaji mzuri kwa kumruhusu mwanamke kuwa Rais.”

