
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohammed Mchengerwa, ametoa agizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, kuacha mara moja kufanya maamuzi kuhusu matumizi ya barabara za mwendokasi bila kibali kutoka wizarani.
Agizo hili limekuja baada ya Chalamila kuruhusu magari binafsi kutumia baadhi ya njia za mabasi yaendayo haraka (BRT) ambazo bado hazijaanza kutumika rasmi.