×

Rais Samia Aleta Mageuzi Sekta ya Afya, Vifo vya Wajawazito Vipungua kwa 80%

KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ally Hapi amesema Rais Dk,Samia Suluhu Hassan amesimama imara kutekeleza miradi ya sekta ya afya na kupunguza vifo vya wanawake wajawazito kwa asilimia 80.

Hapi amesema hayo Jijini Arusha Jijini alipotembelea na kukagua ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje katika hosptali ya wilaya ya Arusha ambalo linajengwa kwa awamu na awamu ya kwanza litagharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.4 na likikamilika litatoa huduma za kibingwa na kibobezi pamoja na utalii wa kimatibabu.

“Hosptali hii yenye hadhi ya nyota tano ni kielelezo Tisha cha kazi kubwa iliyofanywa na Rais Dk, Samia nimezunguka katika mikoa mbalimbali hapa nchini nimejiona kazi kubwa iliyofanywa ya ujenzi wa vituo vya afya vyenye vifaa tiba hadi maeneo ya vijijini”.

Amesema utokana na mafanikio makubwa katika sekta ya afya Rais Dk, Samia amepewa tuzo na taasisi ya Melinda anda Bill Gates ambayo imekuja Tanzania kwa mara ya kwanza”.