×

Rais Samia Azindua Sera Ya Taifa Ya Maji Toleo La Mwaka 2025 (Picha +Video)

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Sera ya Taifa ya Maji 2002, Toleo la 2025 katika Ukumbi wa Mlimani City tarehe 22 Machi 2025, Dar es Salaam.

Rais Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi Sera mpya ya Maji ya Mwaka 2002, toleo la 2025, ikiwa ni sehemu ya hafla ya kilele cha wiki ya Maji iliyofanyika kitaifa katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Sera hiyo ya maji ambayo imekuwepo kwa takribani miaka 23, imezinduliwa ikiwa na
marekebisho kadhaa kwa lengo la kuboresha Sekta ya Maji kwa manufaa ya Taifa, ikiwa ni pamoja na kutambua umuhimu wa sekta binafsi.