
MWENYEKITI Mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ameonekana hadharani leo Machi 25, 2025 baada ya kutoonekana kwa muda mrefu.
Mbowe ameonekana alipohudhuria msiba wa Wilfred Joachim Ngure, ambaye ni baba mkwe wa Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba.
Mbowe ameungana na waombolezaji wengine kuifariji familia ya Mwigulu katika ibada ya kuuaga mwili wa marehemu iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Usharika wa Boko.




