
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Dkt. Charles Kichere, leo Machi 27, 2025 akiwasilisha ripoti kuu kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Charles Kichere amesema Shirika la Reli Tanzania (TRC) limepata hasara ya shilingi bilioni 224 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo limeongezeka kutoka shilingi bilioni 102 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kabla ya kuanza kwa kutumika SGR.
“Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL lilipata hasara ya shilingi bilioni 27.78 mwaka wa fedha 2023/2024 ongezeko hili ni kutoka shilingi bilioni 4.32 ya hasara kwa mwaka uliopita. Hasara hii ya mwaka huu inachangiwa na ongezeko la gharama baada ya kuhamishiwa mkongo wa taifa na kituo cha taifa cha data. Licha ya kukusanya mapato takriban shilingi bilioni 24 kutoka mkongo, fedha hizo hazikuhasibiwa kama mapato ya TTCL badala yake ziliingia kwenye mfuko mkuu wa serikali ili kulipia deni la mkongo. Kutokana na kutopata mapato hayo shirika limeendelea kupata hasara kubwa na kukosa fedha kwa ajili ya Uwekezaji.”
“Kama mapato ya mkongo yangebakia TTCL shirika lingeweza kupunguza hasara kwa takribani asilimia 86% au hata kupata faida kidogo. Napendekeza deni la mkongo wa taifa lilipwe na hazina kama ilivyo kwa madeni mengine ya taifa na mapato yanayopatikana kupitia mkongo huo yaachwe kukusanywa na TTCL ili kuwezesha shirika kujiendesha kiurahisi”
“Napenda kutambua juhudi za serikali kupitia mashirika ya umma ya kibiashara thelathini na moja ambayo yalifanikiwa kupata faida kstika mwamka wa fedha 2023/2024 miongoni mwa mashirika hayo ni Shirika Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC ambayo ilipata faida ya shilingi bilioni 248.75, Shirika la Nyumba la Taifa @nhctanzania shilingi bilioni 242.9 na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA shilingi bilioni 140.48.”
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Dkt. Charles Kichere, leo March 27,2025 akiwasilisha ripoti kuu kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam