×

TANZIA – Balozi Juma Mwapachu afariki Dunia

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kati ya mwaka 2006 na 2011, ameaga dunia Machi 28, 2025  jijini Dar es Salaam.

Balozi Mwapachu alihudumu katika nyadhifa mbalimbali, ikiwemo kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa. Pia alikuwa kiongozi katika sekta ya biashara na maendeleo, ambapo aliwahi kuwa Rais wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).