
Wizara ya Afya imetoa ufafanuzi kuhusu madai ya Neema Kilugala ambaye anadai kubadilishiwa mtoto na kupewa aliyefariki dunia baada ya kujifungua kwa njia ya upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru Machi 24, 2025.
Taarifa kwa umma iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya Afya, Roida Andusamile imeeleza kuwa tayari hatua zimechukuliwa ikiwemo kuchukua sampuli za vinasaba za wanawake waliojifungua kipindi hicho na watoto kwa ajili ya uchunguzi wa DNA.
Pia taarifa hiyo imeeleza kuwa muuguzi aliyemhudumia mwanamke huyo amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi na kwamba taarifa rasmi zitatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.
🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.
