
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) John Mnyika jana Aprili 2, 2025 ametangaza kutengua uteuzi wa Julius Mwita, aliyekuwa Katibu wa Sekretarieti ya Chadema.
Vyanzo vyetu vya kuaminika ndani ya Chadema vinasema kutenguliwa kwa Katibu huyo wa Sekretarieti ya Chadema kumekuja muda mfupi baada ya mzozano mkali ulioibuka mtandaon, ukihusisha makada na wanachama wa Chadema, mara baada ya kuvuja kwa mawasiliano ya kundi sogozi la WhatsApp, lenye viongozi mbalimbali wa sasa, wastaafu na wanachama wa Chadema waliokuwa wakipanga mikakati mbalimbali ya kudhohofisha na kupingana na vuguvugu la Chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania ya No Reforms, No election.

Katika Wingi wa ujumbe wao mfupi uliopigwa picha “screenshot” na kusambazwa kwenye mtandao wa X,na kile kinachotajwa kama ‘huenda’ ndiyo ikawa sababu ya kuenguliwa kwake, Mwita ameonekana akieleza kama ifuatavyo:
“Iko hivi wakuu, ni bora kwenda (Kwenye kikao kilichoitishwa na Chama kikikusisha wanaotaka kuwania Ubunge), tutafute na watu wengine ambao wanaweza kufanya interview (Mahojiano) na Media (Vyombo vya habari) na kutoa maoni tofauti. Sasa tutawakimbia mpaka lini? na ni wapi na kwa namna gani tutaonesha kuwa hatuwaungi mkono?”
Mwita ameendelea kuandika mtandaoni akisema kuwa ” Hiki kikao (Kikao cha Chama na wanachama wanaotaka kuwania ubunge 2025) ni mwiba kwao na kama bosi wao anaona wamemsaliti. Matokeo yakiwa makubwa itakuwa na maana kwamba watu wanaotaka ubunge ni wengi na ikiwa watakasirishwa nao, jamii haitaweza kuwaelewa.”
“Ukiwaacha wakakutana na watu wachache, hisia itakayojengwa ni kuwa watu wameelewa na kuunga mkono No reforms, No election” Hii itajenga tafsiri kuwa UJINGA wao umekubalika kwa kila MwanaChadema na ndio maana hakuna wanaoutaka Ubunge,” ameandika Mwita kwenye moja ya Ujumbe wake uliopigwa picha na kusambazwa mtandaoni.
Stori na Elvan Stambul, GPL