
Klabu ya Simba imemtangaza Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Wallace Karia kuwa Mgeni maalumu kwenye Mchezo wao wa mkondo wa pili wa robo fainali ya kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) dhidi ya Al Masri utakaopigwa Aprili 9, 2025 katika dimba la Benjamin Mkapa.
Akizungumza leo Aprili 4, 2025 kwenye uzinduzi wa Kispika, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo amesema Mgeni maalumu wa mchezo wetu wa robo fainali dhidi ya Al Masry ni Mjumbe wa Kamati Utendaji ya CAF, Rais wa CECAFA na Rais wa TFF, Wallace Karia.
“Tuna kila sababu ya kumpa nafasi hii kwa kutambua mchango wake. Tunatambua, tunaheshimu mchango wa Wallace Karia kwenye mpira wa Tanzania. Simba SC kufika nafasi ya sita kwa ubora Afrika ni katika uongozi wa wake.”—amesema Ahmed Ally