×

Rais Samia Alivyowasili Angola kwa ajili ya Ziara ya Kiserikali ya siku 3 – Picha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan aliwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa 4 De Fevereiro Luanda kwa ajili ya Ziara ya Kiserikali ya siku 3 nchini Angola Aprili 7, 2025.

Rais Dkt. Samia amealikwa na Rais wa Angola João Manuel Gonçalves Lourenço na lengo la Ziara hiyo ni kukuza na kuimarisha zaidi mahusiano ya kihistoria na kidugu baina ya Tanzania na Angola.

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa 4 De Fevereiro Luanda kwa ajili ya Ziara ya Kiserikali ya siku 3 nchini Angola tarehe 07 Aprili, 2025.