
LOS ANGELES, Marekani
MWANAMUZIKI na muigizaji wa Kimarekani, John Legend kweli anampenda mkewe, hii ni kutokana na picha iliyotupiwa mtandaoni akionekana akim ‘kiss’ mkewe Chrissy Teigen ambaye ni mjamzito tumboni.
Legend na Chrissy wanatarajiwa kupata mtoto wao wa kwanza Aprili mwaka huu, hivyo wameonekana kuonyeshana manjonjo ya kumkaribisha.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, wawili hao walionekana wakiwa wametulia nyumbani na kuonyeshana mahaba huku Legend ambaye ni msanii wa muziki, akionekana ‘kupalilia’ zao lao kwa kumbusu mkewe tumboni kabla ya kukumbatiana.