
Klabu ya Yanga Simefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Muungano 2025 baada ya kuibwaga Zimamoto FC ya Zanzibar kwa mikwaju ya penalti 3-1, kufuatia sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za kawaida.
Mchezo ulivyokuwa:
Yanga SC walitangulia kwa bao kupitia kwa Maxi Nzengeli dakika ya 29.
Zimamoto FC wakasawazisha kupitia Said Mwinyi dakika ya 71.
Baada ya muda wa kawaida kumalizika kwa sare, mshindi aliamuliwa kwa mikwaju ya penalti ambapo:
Penalti:
Zimamoto FC: walikosa penalti tatu kati ya nne walizopiga (❌❌✅❌).
Yanga SC: walifunga penalti tatu kati ya nne (✅❌✅✅).
Kwa matokeo hayo, Yanga SC sasa watakutana na JKU FC ya Zanzibar kwenye fainali ya kusisimua ya Kombe la Muungano 2025.
