
Rais wa Jamhuri ya Finland, Alexander Stubb, amewasili jijini Dar es Salaam, Tanzania kwa ziara rasmi ya siku tatu kuanzia Mei 14 hadi 16, 2025. Ziara hii inafanyika kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Wakati wa ziara hiyo, viongozi hao watafanya mazungumzo ya ngazi ya juu yanayolenga kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Finland.
Nchi zote mbili zimejidhatiti kuimarisha ushirikiano kwa kuongeza mahusiano ya kiuchumi na kuchunguza njia mpya za ushirikiano katika maeneo yenye maslahi ya pamoja.




